Friday, October 30, 2009

Kufuatia mauwaji ya alubino mbunge ajitolea kuwajengea nyumba bora na imara.

Florence F. Mrosso


MAUWAJI ya maaalubino hapa nchini Tanzania yalianza kusikika mwishoni mwa mwaka 2007 hali ambayo ilionekana kutikisa nchi kwa kuwauwa binadamu kama mnyama ambae ni kitoweo.


Kufuatia hali hiyo ya mauwaji kwa walemavu wa ngozi (Alubino) mbunge wa kuteuliwa Al-Shymaa Kwegyir ambae pia ni mlemavu wa ngozi alichuchukua jukumu la kutembelea maeneo yanayosadikiwa kuwa na idadi kubwa ya walemavu wa ngozi ili kupata maoni ambayo yanaweza kuwa kizuizi cha walemavu hao kuuwawa.


Muheshimiwa Kwegyir alipowatembelea walemavu wa ngozi waliopo wilaya ya Musoma vijijini alibaini kuwa ili kuthibiti mauwaji hayo kitu cha kwaniza ni ktafuta mbinu za walemavu hao kupata nyumba bopra za kuishi.


“Kwa kutafakari mimi mwenyewe binafaisi nahisi walemavu hawa wanauwawa kwea kuwa wengi wao wana kipato cha chini na pia hawana makazi mazuri ya kuishi,kwani nyumba wanazoishi zikipigwa hata teke tu zinabomoka’’alisema mbunge huyo.


Hata hivyo mbunge huyo wa kuteuliwa hakuishia hapo alichukua jukumu la kutafuta wafadhili watakaowapatia msaada wa kujengewa nyumba walema wa ngozi ili angalau wajistri sehemu imara.

"Walemavu wengi wa ngozio wamekuwa wakiuwawa na kupatwa na majanga haya ya imani za kishirikina hususani mida ya usiku kwa kuwa huishi nyumba ambazo ni za wasiwasi zisizo na uimara wowote"alisema mbunge huyo wa kuteuliwa.


Kwa kuwa aliona kuwa mbunge wa jimbo hilo la msoma vijijini hatashindwa kuwajengea walemavu hao nyumba alimfuata moja kwa moja na kumuomba msaada wa kuwajengea walemavu wa ngozi waliopo katika jimbo lake nyumba bora za kuishi ili kupunguza mauwaji ya walemavu.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Nimrodi mkono hakusita katika kukubali ombi hilo,bali aliridhia kuwajengea walemavu wa ngozi walio katika jimbo lake nyumba bora za kuishi ili kuwaimarishia usalama wa kuishi pamoja na kuwapa malazi bora.


Mbunge huyo alifikia hatua hiyo ya kutaka kuwajengea walemavu hao nyumba baada ya kufikishiwa ombi hilo na mbunge wa kuteuliwa Al-Shymaa Kwegyir kuwa anaomba wenye ulemavu wa ngozi kuhimarisha makazi wanayoishi kwa kile alichodai kuwa nyumba wanazoishi kinaweza kuwa chanzo cha wao kuuwawa kiurahisi zaidi.


Mkono alitoa kauli ya kuwajengea walemavu wa ngozi nyumba bora za kuishi mnamo machi 8 mwaka huu wakati alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Mara yalifanyika kimkoa katika kijiji cha Nyamisisi wilaya ya Musaoma vijijini.


Alisema utekelezaji huo wa kuwajengea utanza mara tu baada ya sensa na kupata idadi kamili ya walemavu hao na kwamba ujenzi wa nyumba hizo utasimamiwa na halmashauri baada ya kutoa fedha za kutekeleza kazi hiyo.


Kwa upande wake mgeni rasmi wa maadhimisho hayo waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Margreth Sitta aliwataka madiwani wa halimashauri zote kupiga vita imani ya mila zilizopitwa na wakati kwa kile alichosema mila hizo ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake na watoto pia ni chanzo cha mauwaji ya walemavu wa ngozi.


Naye waziri mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda alipokuwa akitembelea mikoa ili kubaini chanzo cha mauaji ya alibino alisema kuwa mauwaji haya ni tishio kwa Taifa jambo ambalo alisema kuwa linadhalilisha taifa.


Waziri alisema kuwa watuhumiwa wote wanaokamatwa kuhusiana na mauwaji ya alubino wauwe kwani wanafanya ukatili wa kinyama.


Hadi kufikia mwaka 2009 walemavu wa ngozi zaidi ya 44wameuwawa na watu 3 waliusishwa na mauwaji ya walemavu wa ngozi wamekwisha hukumiwa katika mkoa wa shinyanga.Hukumu waliyopewa watuhumiwa hao ni adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

No comments:

Post a Comment